• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MRADI WA UFYATUAJI MATOFALI ULIVYOSAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI ILEMELA

Posted on: July 9th, 2020

Mradi wa ufyatuaji wa matofali  wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ni mradi ulioibuliwa kwa ajili ya kutanua wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri na hatimae kupunguza utegemezi wa Halmashauri kutoka Serikali Kuu na halikadhalika kuwezesha upatikanaji wa matofali ya ujenzi wa miundo mbinu  katika sekta mbalimbali hususan elimu na afya.

Chimbuko la mradi huu ni mipango ya maendeleo ya halmshauri ya Manispaa ya Ilemela kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani. Katika kupunguza gharama na pia kurahisha ujenzi wa miundo mbinu ya umma.


Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia fedha za makusanyo ya ndani iliamua kununua mashine ya kisasa ambayo iligharimu kiasi cha Fedha za kitanzania shilingi 70,266,000.00.


Lengo kubwa la ununuzi wa mashine lilikuwa ni kuanzisha mradi ya ufyatuaji matofali kwa ajili ya kuzalisha tofali za kukamilisha miundo mbinu ya Elimu na Afya ikiwa ni njia mojawapo ya kuunga mkono jitihada za wananchi kwa kuboresha miundo mbinu ya Elimu na Afya.


Pamoja na hilo pia, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inatarajia kusajili rasmi mradi huu ili uweze kuwa mradi wa kibiashara ambapo utakuwa chanzo mojawapo cha kuingizia mapato katika halmashauri ili kuweza kupunguza utegemezi wa Manispaa ya Ilemela kwa Serikali Kuu katika bajeti ya Maendeleo.


Shughuli za uzalishaji wa matofali zilianza rasmi tarehe 4/2/2020 ambapo hadi kufikia tarehe 30/6/2020 jumla ya matofali 115,292 yenye thamani ya shilingi 135,066,000 milioni yamezalishwa. Kati ya hayo, matofali 63,837 yenye thamani ya shilingi 72,700,700 milioni yamesambazwa  mashuleni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,ukamilishaji wa Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa zahanati ya Nyamadoke,ujenzi wa ofisi ya Kata Bugogwa na matofali 39,955 yameuzwa kwa taasisi jirani .

Mashine hii inayo uwezo wa kufyatua matofali ya inchi sita (6) na inchi tano(5) pamoja  na kuzalisha matofali 5000 kwa siku sawa na asilimia 100 ya uwezo wa mashine. Aidha kutokana na upungufu wa vibao vya kufyatulia matofali kwa sasa huzalisha jumla ya matofali 2500, kutatua changamoto hii halmashauri inafanya utaratibu wa kuagiza vibao vingine.


Yapo mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kupitia mradi huu wa ufyatuaji wa matofali ambayo ni pamoja; Mradi umewezesha kuchangia tofali 63,837 katika ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule 17 za sekondari, shule 4 za Msingi, ofisi ya Kata Bugogwa, Zahanati ya Nyamadoke na Hospitali ya Wilaya ya Ilemela.Pia Mradi umetoa ajira kwa vijana 18 na mama lishe 3 ambao wameweza kujiongezea kipato pamoja na kutoa fursa ya kazi kwa wamiliki 6 wa malori wanaosomba matofali na mchanga katika mradi.


Ununuzi wa mashine hii ya kufyatulia matofali yalikuwa maamuzi ya baraza la Waheshimiwa Madiwani (2015/2020) lililomaliza muda wake na wataalamu wa Halmashauri ya Manispaaa ya Ilemela baada ya kufanya ziara ya kimafunzo katika Jiji la Tanga na kujionea hatua za kimaendeleo zilizopatikana kutokana na mradi wa ufyatuaji wa tofali.




Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.