• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Mhandisi Modest Apolinary akabidhiwa rasmi ofisi Ilemela

Posted on: August 9th, 2021

Mhandisi Modest Joseph Apolinary aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe: Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 01/08/2021 kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela amekabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa hii Ndugu John Paul Wanga leo tarehe 09/08/2021.

Mkurugenzi anaendoka John Wanga mwenye koti jeusi akikabidhi Ilani ya CCM Kwa Mkurugenzi aliyeripoti Mhandisi Modest Apolinary

Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya ya Ilemela, Mstahiki meya na baadhi ya Waheshimiwa madiwani, pamoja na wakuu wa Idara wa Manispaa hii ambapo Ndugu Wanga  amemkabidhi nyaraka na taarifa muhimu kuhusiana na Manispaa ya Ilemela ikiwemo Ilani ya CCM.

Mara baada ya makabidhiano hayo Mkurugenzi anaendoka alipata wasaa wa kuwaaga watumishi wa makao makuu na kuwahimiza kutoa ushirikiano kwa mkurugenzi mpya kwa kufanya kazi kwa uadilifu na ueledi huku akiwashukuru kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote alichokuwepo katika Manispaa hii ya Ilemela.

Pamoja na hayo amemsihi Mhandisi Apolinary kuendeleza yale mazuri aliyoyaacha ikiwa ni pamoja na kuleta matokeo chanya ambayo yatapelekea kuwa  na Ilemela yenye maendeleo.


Kwa niaba ya watumishi wa Manispaa ya Ilemela Ndugu Marco Busungu (Afisa Elimu Msingi), na Ndugu Neema semwaiko(Afisa Kilimo) kwa nyakati tofauti waliahidi ushirikiano kwa Ndugu apolinary, na kumtakia kila la kheri Ndugu Wanga kwa kusema kuwa alikuwa ni mwalimu mzuri kwa watumishi aliowangoza.


Katibu Tawala Ndugu Said Kitinga akiwakilisha kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ilemela alimuahidi Ndugu Apolinary ushirikiano wa kutosha kwani wanajenga nyumba moja huku akimhimiza Mkurugenzi wanga kuwa akaitangaze vyema Ilemela kwa kuendeleza mazuri yake huko anapoenda.

Mhe. Renatus Mulunga ambae ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela alisema kuwa anaamini utendaji wa Mkurugenzi Wanga na kumuahidi Mkurugenzi Apolinary ushirikiano katika kipindi chote atakachokuwepo Ilemela huku akiwasisitiza watumishi wote kuwa kila mmoja asimame katika nafasi yake na kutekeleza majukumu yao.

Mhandisi Modest Apolinary anakuwa ni mkurugenzi wa 3 tangu Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuanzishwa mwaka 2012 nae amewaomba watumishi ushirikiano ili kuweza kuzitatua changamoto mbalimbali katika Manispaa hii ya Ilemela hususan za wananchi.


Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.