• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA AKABIDHI SARUJI NA CHOKAA KWA MANISPAA YA ILEMELA

Posted on: January 24th, 2019

Mbunge wa jimbo la  Ilemela, Mhe Dkt Angeline Mabula, leo tarehe 24.01.2019 amekabidhi jumla ya  mifuko ya saruji 700 na mifuko 1200 ya chokaa kwa uongozi wa Manispaa ya Ilemela.


Akikabidhi saruji na chokaa hiyo kwa uongozi wa Manispaa ya Ilemela , katibu wa Mbunge kwa niaba yake Mbunge amesema kuwa Mhe Mbunge ameelekeza kuwa saruji na chokaa hiyo itumike katika ujenzi wa madarasa ya Shule za sekondari Ilemela kwani upungufu wa madarasa ni mkubwa kutokana na ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba 2018.

Pamoja na hayo Mbunge ametoa shukrani za kipekee kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga  Mhe.Martine Shigela kwa ushirikiano wake mkubwa katika kufanikisha kupata msaada huo, pia ameishukuru kampuni ya usafirishaji  ya Z.B MINING LTD kwa kusafirisha saruji na chokaa hiyo.


Ndugu Jonex Joel, mwakilishi kutoka kampuni ya TEXAS ambae ni wakala kwa kanda ya ziwa amesema kuwa, ufadhili  huo umetolewa ikiwa ni katika kuunga juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mhe Mbunge wa Jimbo la Ilemela katika kuwaletea maendeleo wananchi.

“Tumeona upo umuhimu wa kuunga juhudi za Mbunge kwani amekuwa mstari wa mbele katika kutafuta misaada mbalimbali kwa ajili ya wananchi  wa Ilemela pia tunawakaribisha kuleta maombi mengine kama lipo ndani ya uwezo wetu tutatoa”, Alisema


Mstahiki Meya wa Ilemela, Mhe.Renatus Mulunga nae amemshukuru Mbunge kwa jitihada zake mbalimbali katika kutatua changamoto katika jimbo la Ilemela,kwani mbali na kutafuta saruji na chokaa amekuwa ni msaada mkubwa kwa kutoa matofali kwa ajili ya ujenzi wa maboma kwa shule za Ilemela.

“Ukitaka nchi iendelee wekeza kwenye elimu, na dhamira kuu ni kutaka kuona Ilemela inatoka hapa ilipo na ndio maana Ilemela inatumia njia ya ushirikishaji kuanzia ngazi ya jamii ambapo wananchi wanajenga msingi, mbunge anajenga boma kwa kutoa matofali na kisha Manispaa inakamilisha jengo kwa kuezeka”, alisema


Nae Ndugu John Wanga, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, amesema kuwa saruji  na chokaa ina manufaa makubwa katika kukabiliana na changamoto ya ujenzi wa madarasa na hili limetokana na ufaulu mkubwa Ilemela kwa wanafunzi waliomaliza darasa la saba mwaka 2018.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa, Mbunge ameendelea kutembea na kauli mbiu , “mrithishe elimu mtoto na sio mali”, kwa  kuhakikisha kuwa madarasa yanakamilika na kwa jitihada hizi atatimiza ndoto ya kuwekeza elimu kwa mtoto.


Mifuko 700 ya saruji imefadhiliwa na Kampuni ya Kilimanjaro Cement na Kampuni ya Neelkanch Chemical Ltd imetoa mifuko 1200 ya chokaa ikiwa ni jitihada za Mbunge wa Ilemela katika kutatua changamoto za ujenzi wa madarasa.





Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.