• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

KITUO CHA MICHEZO SABASABA-ILEMELA CHAZINDULIWA RASMI

Posted on: October 15th, 2019

“Nichukue fursa hii kuonyesha furaha yangu ya dhati nikiwa kama mwanamichezo kwa  kukamilika kwa ujenzi wa kituo hiki cha michezo, kwani huu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala wa kuendeleza michezo Tanzania” ,Haya yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongela alipokuwa akihutubia kadamnasi iliyofika kushuhudia uzinduzi wa kituo hicho.


Akizindua kituo hiki Mhe. Mongela, ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuhakikisha kuwa, inaweka nguvu zaidi katika kulipendezesha eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa inaweka uzio kwani ukitaka kubebwa ni lazima ubebeke, Alisistiza


Aliendelea kusisitiza kuwa wana michezo wote kuunga mkono wito wa taasisi ya Sport Charity kuwa jamii inatakiwa ijitokeze kufanya mazoezi katika viwanja hivi ili wafadhili wapate moyo wa kuendelea kufadhili.


Pamoja na hayo ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji ili kuweza kukamilisha ujenzi wa eneo hilo  na kuahidi kuendelea kutafuta wafadhili mbalimbali kwa ajili ya kukiendeleza kiwanja hiki.


Kituo hiki ambacho kimefika takribani asilimia 90 za ukamilishaji kimegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Milioni mia moja na sitini kinajumuisha viwanja vinne vya michezo ambavyo ni kiwanja cha mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa pete pamoja na mpira wa kikapu.


“Akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hiki kwa mgeni rasmi, Ndugu Isack Mwanahapa ambae ni katibu wa taasisi ya “Sports Charity”, ametoa shukurani kwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa kukubali kutoa eneo hilo ili liweze kutumika kwa ajili ya michezo.


Pia alimshukuru Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe.Dkt.Angeline Mabula kwa jitihada zake za kufuatilia  kwa karibu na kutoa msaada mara zote unapohitajika pamoja na kutoa hamasa ya ujenzi kwa kuchangia tofali takribani 1000.


Pamoja na shukurani hizo alizozitoa, aliomba kutatuliwa kwa changamoto mbalimbali kubwa hasa ikiwemo eneo la kituo hicho cha michezo kutumika na wafanyabishara hasa siku yam nada jambo ambalo linaweza kudhoofisha uboreshaji wa kiwanja hicho pamoja na kupelekea nyasi na miti kutokustawi na pia litaharibu ubora wa uwanja huo.


Nae Naibu Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mhe.Wilbard Kilenzi ambae pia ni diwani wa kata ya Ilemela ambapo kituo hicho kimejengwa akitoa shukurani zake amewaomba wafadhili kufikiria suala la kuleta walimu wenye taaluma ya michezo, kwani vipaji vipo vingi ila inashindikana kuvikuza kutokana na ukosefu wa wataalam wa kutosha wa michezo.


Mhe.Dkt Angeline Mabula, Mbunge wa Ilemela amewashukuru wafadhili hao kwa kufanikisha ujenzi wa kituo hicho na huku akisisitiza uwepo wa timu nyingi na za kutosha ili kuweza kufanya mazoezi kwani michezo ni afya na pia uwepo wa kituo hicho cha michezo itapunguza vijana kukaa vijiweni italeta ajira huku akiwataka wana Ilemela kujitokeza kwa wingi kutumia viwanja hivi.


Bi Estelle Brulhart, mwakilishi wa wafadhili kutoka ujerumani, ufaransa,uswizi wakiwemo wanafunzi na watu binafsi, amewashukuru wote walioshiriki katika ujenzi wa kituo hiki na kusema kuwa anaendelea kuwatia moyo wachezaji kuendelea kufanya mazoezi kwani michezo ni afya.


Akihitimisha , Afisa Tarafa ya Ilemela Ndugu Mzava  kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuendelea kuielea Ilemela na pia kwa msaada aliotoa wa mifuko ya saruji huku akitoa maelekezo kwa wafanyabiashara wanaotumia eneo hilo siku ya mnada kuhamia eneo lingine ambalo wataonyeshwa ili kupisha eneo la viwanja hivyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa viwanja hivyo vinatunzwa na kulindwa ili viweze kudumu kwa muda mrefu.


Hiki ni kituo cha pili kujengwa na taasisi ya Sports Charity Mwanza kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali wa michezo kutoka nchi za Ujerumani,Ufaransa, na Uswisi Kukamilika kwa uwanja huu kutasaidia kuibua vipaji mbalimbali katika sekta ya michezo, kutengeneza ajira kwa vijana na jamii kwa ujumla, pia kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa.



Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.