• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

ILEMELA KUKUSANYA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 8.8 KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020

Posted on: January 16th, 2019

Katika mwaka wa fedha 2019/20 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inakadiria kukusanya jumla ya Tsh.8,878,387,000. 00 kutoka vyanzo vya ndani. Sababu zilizopelekea kufikia makisio haya ni pamoja na takwimu halisi zilizokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali, mwenenendo wa ukusanyaji mapato kutoka vyanzo mbalimbali kwa miaka ya nyuma, mabadiliko ya sheria mbalimbali yanayohusu tozo na kodi mbalimbali.


Chanzo hicho cha ndani, kinafanya jumla kuu ya makisio ya bajeti ya mapato kutoka katika vyanzo vya ndani na serikali kuu kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kuwa kiasi cha Shilingi 75,891,541,247.98 za kitanzania, ambapo ruzuku ya miradi ya maendeleo imekisiwa kuwa kiasi cha Shilingi 23,453,644,376.00,ruzuku ya matumizi ya kawaida ikiwa Shilingi 2,011,687,870.98, mishahara Shilingi 41,547,622,000.00 na mapato ya ndani shilingi 8,878,487,000.00


Makadirio ya bajeti hii kwa mwaka wa fedha 2019/2020 yamelenga katika matumizi ya kawaida pamoja na matumizi ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Aidha maeneo ya vipaumbele kwa bajeti hiyo yameainishwa kuwa ni pamoja na sekta ya  ujenzi ,afya,utawala,elimu sekondari na msingi, Maendeleo ya jamii, ardhi na mmipangomiji maji, uvuvi na mifugo, usafishaji na mazingira, kilimo pamoja na misitu na nyuki.


Kwa upande wa ujenzi shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi  na ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami na changarawe,kwa upande wa sekta ya afya shughuli zitakazotekelezwa ni ukamilishaji wa ujenzi wa hospitali ya wilaya, utoaji wa huduma za lishe na uboreshaji wa huduma za afya katika vituo vya afya 3 na zahanati 13.


Aidha shughuli zitakazotekelezwa katika sekta ya utawala ni ujenzi wa jengo la utawala, pamoja na uboreshaji wa majengo yalipo kwenye katika halmashauri ikiwemo ofisi za kata.Elimu Msini na Elimu sekondari shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari sangabye, ujenzi wa ofisi na nyumba za walimu na vyumba vya madarasa pamoja na uboreshaji wa miunombinu ya shule.


Katika sekta ya maendeleo ya jamii fedha zitaelekezwa katika miradi ya kudhibiti UKIMWI na uwezeshaji wa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu. Sekta ya ardhi na mipangomiji itatekeleza shughuli za uthamini, upimaji wa viwanja ikiwa ni pamoja na ulipaji wa fidia na uendelezaji wa eneo maalum la ukanda wa kiuchumi.


Shughuli zitakaotekelezwa katika sekta maji ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa maji safi na salamakatika maeneo ya pembezoni kwa kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya maji.Pamoja na hayo sekta ya uvuvi imejipanga kutekeleza shughuli za  ukarabati na umaliziaji wa miundombinu katika machinjio ndogo za Igombe na Kayenze, uboreshaji wa mialo yote pamoja na ujenzi w daraja la kupandia na kushukia abiria kwatika mwalo wa Kirumba.


Halikadhalika sekta ya usafishaji na mazingira imejipanga kuimarisha usafi na mazingira kwa kuondoa taka ngumu kwa kushirikisha jamii.Kwa upande wa kilimo sekta imejipanga kujena jengo la kusindika unga wa mhogo katika kata ya Kayenze pamoja na kutoa mafunzo na kukabiliana na majanga mbalimbali.Katika sekta ya Nyuki/Misitu ilemela itahakikisha inatoa elimu ya mazingira, kuotesha miche ya miti pamoja na kutengeneza mizinga ya nyuki na kuigawa kwenye vikundi.


Zipo changamoto mbalimbali ambazo halmashauri imekuwa ikikabiliana nazo katika katika kutekeleza majukumu yake ni pamoja na uwezo mdogo wa Halmashauri katika kutoa huduma za kijamii hasa katika sekta ya  Elimu, Afya, Maji na Miundombinu kutokana na ufinyu wa Bajeti ikilinganishwa na mahitaji,.

Hivyo katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika Halmashauri, mikakati ya kuongeza mapato ya vyanzo vya ndani imewekwa ili kuhakikisha kuwa mapato yanakusanywa kwa ufanisi ili kufikia malengo ya kutekeleza shughuli mbalimbali kwa kuongeza uwezo wa halmashauri kujitegemea.


Baadhi ya mikakati ni pamoja na, kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa mapato na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, kupitia Sheria ndogo za Halmashauri za mapato ili kufanya marekebisho ya viwango vya ushuru na kodi, Kuendelea kutoa elimu kwa mawakala na walipa kodi kuendelea kuimarisha mfumo wa utunzaji takwimu na kumbukumbu za walipa kodi, Kuchukua hatua zaidi za kisheria kwa wanaoshindwa kulipa ada na tozo mbalimbali za Halmashauri, Kuongeza idadi ya mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato katika vyanzo vyote, Maandalizi ya mradi wa  kimkakati wa “Nyamhongolo Bus and Truck Terminal, Maandalizi ya Mpango Kabambe wa eneo la uwekezaji (industrial Park) eneo la Nyamhongolo uko kwenye hatua za mwisho za kukamilika. Kushirikiana na Wahisani (World Bank, UNCDF) katika uboreshaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya vyanzo vya mapato kama vile Masoko, Jengo la Machinga na Nyumba za Makazi.


Kwa mwaka huu wa fedha 2018/19 ,Ilemela ilijipanga kukusanya kiasi cha Shilingi za kitanzania 9,024,065,000.00 ambapo mapato halisi yaliyokusanywa hadi kufikia Desemba 2018,  ni Shilingi 3,818,961,26.78 sawa na asilimia 42.3.


Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.