• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

HARAMBEE YA UCHANGIAJI MADAWATI ILEMELA YAENDELEA KUZAA MATUNDA

Posted on: October 11th, 2022

Harambee ya uchangiaji wa madawati kwa shule za Msingi Ilemela iliyofanyika takriban miezi minne iliyopita imeendelea kuzaa matunda ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala amepokea jumla ya madawati 50 yaliyogharimu shilingi milioni 4 kutoka kwa benki ya NBC-Mwanza.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya madawati hayo Mhe.Masala amesema lengo la Wilaya ya Ilemela ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi anakaa chini sambamba na kuwapatia watoto mazingira bora zaidi ya kujifunza na kujifundishia .

Aidha Mhe.Masala ametoa shukrani kwa benki ya NBC kwa niaba ya timu nzima ya Ilemela kwa kutimiza ahadi yao huku akiwaomba kuendelea kuunga juhudi mbalimbali za maendeleo hususan kuunga mkono zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa linaloendelea kwa shule za msingi za Manispaa ya Ilemela.


“Natambua ushiriki wa benki ya NBC katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo wilayani kwetu,nami nawaahidi kuwa itakapojitokeza fursa ya sisi kufanya kazi na ninyi kupitia huduma mbalimbali za kibenki mnazotoa tutafanya kazi.” Amesema Mhe.Masala.


Meneja wa benki ya NBC-Mwanza ndugu Thomas Lijaji ameeleza kuwa utoaji wa madawati hayo ni moja ya huduma wanazozitoa kwa jamii ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii hususan Wilaya ya Ilemela ambayo pia ni kati ya wateja wake wanaoendelea kupata huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo mikopo ya kuwainua kiuchumi


“Sisi kama NBC tuliahidi madawati 50 na leo tumekuja kuyakabidhi na hatujafunga milango ya kushirikiana na jamii na pale mtakapokuwa na mahitaji yoyote niendelee kuwakaribisha tupo tayari kuendelea kushirikiana nanyi”amesema Ndugu Lijaji

Mhe. Renatus Mulunga Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela akitoa shukurani zake kwa benki ya NBC amewataka walimu na wanafunzi kuhakikisha wanatunza miundombinu hiyo ya madawati ili hata waliochangia waendelee kupata moyo wa kuchangia huku akisisitiza kuendelea kuishi katika kauli mbiu ya Ilemela inayosema “Ilemela  ni yetu tushirikiane kuijenga”.


Neema Richard Charles mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Kaselya amewashukuru NBC kwa kutoa madawati hayo kwani inaenda kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati huku akiwaomba wasichoke kuendelea kuwasaidia.


Madawati haya 50 yanaenda kupunguza  changamoto ya watoto 150 kukosa madawati hili ni jambo kubwa sana kwetu pamoja na hilo tuwaombe tena kutushika mkono  katika utatuzi wa changamoto ya vyumba vya madarasa kwa shule za Msingi amesema, Mhandisi Modest Apolinary Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela.





Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.