• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MANISPAA YA ILEMELA YATARAJIA KUKUSANYA TSHS. 9,024,065,000.00 KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019

Posted on: February 28th, 2018

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inatarajia kukusanya kiasi cha Tsh 9,024,065,000.00  kutoka katika vyanzo vyake vya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Ndugu John Wanga alipokuwa akiwasilisha makisio na mpango wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha 2018/2019 katika Baraza la Waheshimiwa madiwani.

Aidha alisema kuwa kushuka kwa makisio ya mpango na bajeti hiyo kumetokana na kuwa vyanzo vilivyokuwa vikikusanywa na halmashauri  kuelekezwa kukusanywa na serikali kuu chini ya usimamizi wa Mamlaka ya mapato (TRA) jambo ambalo limepelekea bajeti ya Halmashauri kupungua kwa asilimia 23 ambayo ni sawa Tshs 2,729,545,000/= ya bajeti.


Aliendelea kwa kusema kuwa endapo vyanzo hivi vingekuwa chini ya Halmashauri bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa upande wa mapato ya ndani makisio yangefikia Tshs 13,119,065,000.00 kwa ongezeko la Tshs 4,095,000,000.00 sawa na asilimia 17 ya bajeti ya sasa.


Sambamba na hilo Mkurugenzi alisema kuwa, ili kuongeza mapato ya ndani, halmashauri imejiwekea mikakati mbalimbali  kuhakikisha kuwa mapato yanakusanywa kwa ufanisi kuweza kufikia malengo yaliyowekwa ikiwa ni pamoja na ununuzi wa magari 3,uboreshaji wa miundombinu ya barabara kupitia wakala wa barabara (TARURA), kuboresha majengo ya kutolea huduma za afya na elimu.Halikadhalika imelenga kuboresha miundombinu ya mialo na masoko,pia kupitia kauli mbiu ya Wilaya “Ilemela ni yetu tushirikiane kuijenga”, wannachi wataendelea kuhamasishwa juu ya uchangiaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wahisani na wadau wa maendeleo.


Nae Naibu Meya wa Manispaa ya Ilemela Mhe.Wilbard Kilenzi kwa niaba ya Mstahiki Meya aliwashukuru watendaji kwa maandalizi mazuri ya mpango na bajeti na kuwataka kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kujituma ili  kutekeleza yale yote yaliyopangwa  ili kuweza kufikia malengo ambayo yamewekwa.

Jumla ya kiasi cha Tsh. 68,613,400,00.00 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 zilipitishwa na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jana tarehe 27/02/2018 ambapo kati ya fedha  hizo Tshs. 15,013,332,000.00 ni fedha za ruzuku ya miradi ya maendeleo, Tshs 1,620,686,000.00 ni fedha za ruzuku ya matumizi ya kawaida, Tshs. 42,75,317,000.00 ni kwa ajili ya mishahara, na Tshs. 9,024,065,000.00 ni fedha ya mapato ya ndani.




Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.