• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

BARAZA LA MADIWANI ILEMELA LAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA PILI

Posted on: January 30th, 2025

BARAZA LA MADIWANI ILEMELA LAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA PILI

 

Baraza la madiwani Ilemela likiongozwa na mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mhe.Renatus Mulunga limepongeza taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili ( Oktoba - Desemba ) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo inayoonyesha kata zote 19 zinazounda Manispaa hiyo kupata mgao katika kutekeleza miradi yao.

 

Akitoa taarifa ya mkurugenzi  wakati wa kikao hicho kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ndugu Egidy Teuras amesema Manispaa ya Ilemela imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 7.01 sawa na asilimia 47 ya lengo la mwaka  na sawa na asilimia 93.8 ya lengo la nusu mwaka wa fedha 2024/2025.

 

Ndugu Egidy ameongeza kwa kusema kuwa kiasi cha shilingi milioni 270.96 fedha za mapato ya ndani zimetumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya kata 19 za manispaa ya Ilemela katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2024/2025

 

Nae katibu tawala wa wilaya ya Ilemela, wakili Mariam Msengi amechangia kwa kusema kuwa masuala ya ukusanyaji mapato ni muhimu kwa wilaya yetu kwani yataiwezesha manispaa kufikia malengo yake ya utekelezaji wa miradi sambamba na kuwahudumia wananchi wetu na kuwaletea maendeleo ambayo ni kiu ya kila mtu.

 

Akijibu swali la Mhe.Issa Mwalikila Diwani wa kata ya Kayenze lililohoji kuhusu mpango wa dharura wa TARURA katika utengenezaji wa barabara ya kuelekea Lukobe kata ya Kahama, meneja wa TARURA Mhandisi Sobe Makonyo amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 2.15 imekwisha kamilika kwa marekebisho yaliyofanyika kwa kutumia magreda ya Manispaa ya Ilemela shughuli iliyotekelezwa mnamo Januari 28 ,2025.

 

Akihitimisha baraza hilo Mhe.Mulunga amewaasa wanaIlemela kupeleka watoto shule kwa kuzingatia umuhimu wa elimu katika maisha ya kila siku huku akimuagiza mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha anaweka mpango wa kuanza kujenga madarasa ya maghorofa.

 

"Ujenzi wa madarasa ya maghorofa utatuwezesha kutumia ardhi yetu vizuri,majengo mengi katika eneo dogo."

Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.