• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

BARAZA LA MADIWANI ILEMELA LAHIMIZA ULIPAJI WA FIDIA KWA MAENEO YALIYOTWALIWA NA HALMASHAURI

Posted on: February 2nd, 2024

Baraza la madiwani limemuelekeza mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Wakili Kiomoni Kiburwa Kibamba kuhakikisha kuwa analipa fidia katika maeneo yote yaliyotwaliwa na manispaa hiyo kwa shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili yaweze kumilikiwa na umma.

Rai hiyo imetolewa na Mstahiki Meya Mhe Mulunga wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichoketi kwa ajili ya kujadili taarifa za utekelezaji katika kipindi cha robo ya pili yam waka wa fedha 2023/2024 (Oktoba  hadi Disemba) ambapo amefafanua kuwa upo umuhimu mkubwa wa  kutwaa maeneo kwa kulipa fidia  na kuyalinda kwa ajili ya shughuli za umma kama ujenzi wa vituo vya afya, zahanati na shule


“ Niwapongeze na kuwashukuru viongozi waliokuwepo wakati Hayati Mwalimu Nyerere anatangaza vijiji vya ujamaa ambapo maeneo kama ya Sangabuye wakachukua eneo kubwa sana, wasingechukua maeneo makubwa hata ile sekondari ya Sangabuye isingekuwepo, Mkurugenzi tumia maarifa yako yote, uwezo wako wote, sheria zako zote hakuna kuachia hata kipande cha ardhi tulichokitwaa.” Alisema Mhe Mulunga


Aidha Mhe Mulunga amewaasa viongozi kufikiria vizazi vijavyo pindi wanapopanga mipango ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo pamoja na kutanguliza maslahi ya umma badala ya kujifikiria wao binafsi ili vizazi vijavyo viweze kunufaika na rasilimali za nchi zilizopo


Akichangia mjadala huo, Wakili Wilbard Kilenzi diwani wa kata ya Ilemela alishauri baraza la madiwani la kuhakikisha linasimamia msimamo wa kutorejesha maeneo yaliyotwaliwa kwa shughuli za umma kwa kuwa kufanya kinyume chake ni kuiingiza Manispaa hasara kwani itapaswa kulipa gharama zaidi za fidia kwa waliotwaliwa maeneo yao kutokana na kuwasitishia kuendeleza maeneo yao kwa muda mrefu  na hivyo kusisitiza juu ya suala la ulipaji wa fidia kwa maeneo hayo yaliyotwaliwa.


Baadhi ya madiwani kwa nyakati tofauti walishauri kuwa ni vyema halmashauri ikaweka utaratibu wa kutenga fedha kila mwezi kwa ajili ya malipo ya fidia ili kuondokana na deni hili.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela wakili Kiomoni Kibamba alifafanua hoja hiyo kwa kusema, kuwa zaidi ya shilingi bilioni 5.9 zinadaiwa na wananchi kwa ajili ya fidia kutokana na Serikali kutwaa maeneo yao kwa shughuli mbalimbali za maendeleo na kwamba Manispaa yake itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya fidia hizo na kusema kuwa kwa maeneo yote ambayo yameshapimwa hayatarudishwa kwa wananchi.


"Maeneo yote ambayo tulikwisha kuyapima hayatarudishwa aidha tunahitaji kuchukua maeneo zaidi na tayari nimemuelekeza Mchumi kuandika andiko la kuomba mkopo ili tuweze kuchukua maeneo zaidi, na halmashauri itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kulipa fidia na kuzidi kibuni vyanzo vya fedha ili kuweza kulipa deni lote la fidia”. Ndugu Kibamba alifafanua


Hata hivyo Wakili Kibamba alisema kuwa hadi sasa Halmashauri imefanikiwa kulipa fidia kiasi cha shilingi Bilioni 1.3  kwa wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya mradi wa upimaji eneo la Nyafula, barabara za Buswelu – Nyamadoke chini ya mradi wa TACTIC, pamoja na taasisi za umma kama vile shule za msingi na sekondari.







Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.