• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

BAJETI YA SHILINGI BILIONI 81.45 YAPITISHWA NA BARAZA LA MADIWANI ILEMELA, WAHIMIZA UTEKELEZAJI

Posted on: February 1st, 2024

Baraza la madiwani wa Manispaa ya Ilemela limeijadili na kuipitisha rasimu ya mpango na bajeti ya mwaka 2024/2025 ya kiasi cha shilingi Bilioni 81.45 kwa ajili ya matumizi ya Manispaa ya Ilemela ambayo itajumuisha ,mishahara ya watumishi ,ruzuku ya miradi ya maendeleo, ruzuku ya matumizi ya kawaida, miradi ya maendeleo na mapato ya ndani.


Wakiijadili bajeti hiyo katika nyakati tofauti waheshimiwa madiwani wamepongeza kwa namna ambavyo bajeti hiyo inaenda kugusa sekta mbalimbali, huku wakihimiza kuwa isiwe bajeti ya kuishia kwenye makaratasi bali iwe ni bajeti inayotekelezeka.




Sambamba na hilo, Madiwani hao wametilia mkazo suala la ukamilishaji wa miradi viporo hususan ambayo ilianzishwa na wananchi ili kuweza kuunga juhudi za wananchi na kuwatia moyo kuendelea kushiriki katika uanzishaji wa miradi mipya na shughuli za maendeleo kwa ujumla


Akiwasilisha rasimu ya mpango na bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela,  Ndugu Herbert Bilia ambae ni Mchumi wa Manispaa alibainisha kuwa kupitia chanzo cha mapato ya ndani halmashauri  inayo mpango wa kuanzisha shule za Sekondari  mbili za mfano katika kata za Buswelu na Ilemela sambamba na maboresho ya miundo mbinu mbalimbali katika sekta ya zote.


“Katika vipaumbele vilivyoletwa kutoka katika kata kupitia WDC mahitaji makubwa ni sekta za afya, elimu sekondari na msingi, kwa kuliona hilo, kupitia mapato ya ndani katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa upande wa elimu tunatarajia kujenga shule mbili za sekondari za mfano katika kata za Ilemela eneo la Lumala na Kata ya Buswelu kufuatia kwamba maeneo hayo yamezidiwa na idadi kubwa ya wanafunzi”, Alisema Ndugu Bilia.


Kwa upande wa sekta ya Afya Ndugu Bilia aliendelea kufafanua kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kupitia mapato ya ndani Halmashauri inatarajia kujenga kituo cha afya katika kata ya Ibungilo ili kupunguza msongamano katika kituo cha afya Buzuruga.

Aidha alisema kuwa Halmashauri inatarajia kutumia fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 2.3 kwa ajili ya sekta ya miundombinu ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi Bilioni 1.1 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa barabara katika kata zote 19 za Manispaa ya Ilemela, ambapo Halmashauri kupitia mapato ya ndani inaendelea na mchakato wa manunuzi ya mitambo ya kisasa kwa ajili ya matengenezo ya barabara.


Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Renatus Mulunga amehitimisha kwa kuhimiza  juu ya suala la utekelezaji wa bajeti hiyo na kuwataka watendaji kwenda kuisimamia ipasavyo kwa ajili ya maendeleo ya Ilemela huku akihimiza juu ya suala la ushirikiano


“ Kupitisha bajeti ni suala moja, na utekelezaji wa bajeti ni suala jingine twendeni tukaisimamie iweze kutekelezeka” alihitimisha


Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.