Kata ya Nyamanoro ni miongoni mwa kata 19 zinazounda Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela. Kata hii ina jumla ya mitaa 7 ambayo ni Nyamanoro Mashariki, Nyamanoro “A”, Mkudi, Nenetwa, Mnyampala, Kilimahewa “A”, na Kilimahewa “B”. Kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2022, kata ya nyamanoro ina jumla ya wakazi(watu) 24624 ikiwa wanaume ni 11751 na wanawake ni 12873 na tofauti kati ya wanaume na wanawake ni 1122.
SHUGHULI KUU ZA KIUCHUMI,
wakazi wengi wa kata hii wanajishughulisha na shughuli za biashara ndogondogo na kubwa, ajira za serikalini na taasisi binafsi na pia ufugaji kwa kiwango kidogo.
ELIMU
Sekta hii imegawanyika katika maeneo mawili ambayo ni elimu msingi na elimu sekondari. Kwa upande wa elimu msingi, kata inazo jumla ya shule 5 za serikali ambazo ni Mkudi, Mjimwema, Ghana, Karume, na pia shule ya Mwenge. Shughuli zilizotekelezwa kwa kipindi hiki ni pamoja na kufundisha na kujifunza pamoja na usimamizi wa mitihani mbalimbali ya majaribio. Kata ya nyamanoro Ina jumla ya shule 06 ambapo ni shule tano na msingi na shule moja nisekondari, shule zote ni za serikal
Mhe.G. MAGANIKO I.E. -DIWANI
HOSEA M/KITI KATIBU- MTENDAJI WA KATA
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.