UTANGULIZI
Kata ya Nyakato ni kati ya kata 19 zinazounda Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela. Kata ya Nyakato in jumla ya Kaya 8,131 mitaa 8 yenye jumla ya wakazi 29,560 ambapo wanawake ni 15,717 na wanaume 13,843 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022.
UONGOZI NA UTAWALA
Kata ya Nyakato ina uongozi kama ifuatavyo:- Mhe. Diwani, Afisa Mtendaji Kata, Afisa Elimu Kata, Afisa Afya 1, Afisa Mifugo, Afisa Kilimo 2, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Ustawi na maafisa wa mitaa 4 wa kuajiriwa na 2 wa kujitolea na wenyeviti wa mitaa 8 (Mheshimiwa Diwani na wenyeviti wote 8 wanatokana na Chama cha Mapinduzi).
HALI YA UCHUMI
Wakazi wa Kata ya Nyakato sehemu kubwa ni wafanyabiashara ndogo ndogo, wafanyakazi viwandani yaani katika viwanda vikubwa na vidogo, maofisini na sehemu ndogo ni wakulima wa bustani na ufugaji mdogo. Pia kuna vikundi vinavyofanya biashara ya pesa kupitia kuweka na kukopa na kuuza hisa
DIWANI: MHE Jonathan M. Mkumba
MTENDAJI WA KATA Juma M. Ngoroma Mwenyekiti Katibu
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.