Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumatano ya tarehe 27 Novemba 2024, jumla ya wasimamizi wa vituo 986 ndani ya halmashauri ya manispaa ya Ilemela wameapa kiapo cha utii.
Kiapo hicho cha utii kimeenda sambamba na mafunzo yaliyolenga kuwapatia elimu na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kutekeleza majukumu yao ili kufanikisha uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024
Nae bi Doreen Ntongani Afisa TAKUKURU ilemela amewakumbusha wasimamizi hao kuwa ni jukumu lao kuzuia vitendo vya rushwa na kutoa taarifa waonapo viashiria vya rushwa.
Akifunga mafunzo hayo Msimamizi w Uchaguzi Manispaa ya Ilemela amewahimiza wasimamizi wa vituo kuhakikisha kuwa mitaa yote ya Ilemela inapiga kura siku ya uchagu na isitokee mtaa ukashindwa kupiga kura.
"Nitoe rai kwenu kuhakikisha kila mtaa unapiga kura matokeo yatangazwe siku hiyo hiyo ya uchaguzi mara baada ya zoezi kukamilika"amesema Bi Ummy
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.