Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 27 Novemba 2024, msimamizi wa uchaguzi manispaa ya Ilemela Bi Ummy Wayayu ameendelea kukutana na makundi mbalimbali, ambapo leo tarehe 19 Novemba 2024 amekutana na viongozi wa vikundi vya kijamii vilivyopo Ilemela.
Lengo ikiwa ni kutoa hamasa kwa wananchi wa Ilemela kujitokeza katika kampeni za wagombea wa vyama 15 vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na kusikiliza sera zao ili itakapofika siku ya uchaguzi waweze kuchagua viongozi sahihi watakao waletea maendeleo katika mitaa yao.
Pamoja na hilo amewataka viongozi hao wa vikundi vya kijamii kuwahimiza wanachama wao kuhakikisha wanatunza amani na kutokuwa miongoni mwa watakaotumika kuvunja amani ya nchi pamoja kutoa taarifa mara moja patakapotokea viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Nae afisa uchaguzi wa Manispaa ya Ilemela Ndugu Shilinde Malyagili amewakumbusha viongozi hao kuwa siku ya uchaguzi itakuwa ni siku ya mapumziko hivyo wakawahimize wanachama wao pamoja na familia zao kujitokeza kupiga kura kwa kuchagua viongozi watakaowafaa kwa miaka mitano ijayo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.