Kata ya Kirumba ni miongoni mwa Kata kumi na tisa (19) zinazounda Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela. Kata hii ina jumla ya Mitaa kumi na mbili (12) mitaa hiyo ni (i) Mlimani (ii) Kiyungi (iii) Ngara (iv) Kirumba Kati (v) Magomeni (vi) Ibanda juu (vii) Mlimani ‘’B’’ (viii) Kabuhoro (ix) Kabuhoro ‘’B’’ (x) Ibanda Busisi (xi) Ibanda Ziwani na (xii) Kigoto.
UONGOZI WA UTAWALA
Mhe. Diwani Wessa Juma Nabahani (kupitia Chama cha Mapinduzi)
Afisa Mtendaji wa Kata
Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC)
Wataalamu ngazi ya Kata
Watendaji wa Mtaa
IDADI YA WATU
Kata ya Kirumba ina jumla ya wakazi 32,364 kati ya hao wanaume ni 15,693 na wanawake 16,671 Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
HALI YA UCHUMI
UVUVI
Eneo hili kutokana na kuzungukwa na maji hasa maeneo ya Mwaloni, Kigoto, Ibanda Ziwani na Ibanda Busisi wakazi wake wanajishughulisha zaidi na shughuli za uvuvi na kujipatia kipato kata ya kirumba ina jumla ya wavuvi 423 na ina Mitumbwi 54 ambapo kati ya hiyo Mitumbwi 21 ndiyo iliyosajiliwa.
Kata ya Kirumba wakazi wake wengi pia wanajihusisha na Biashara kwa kuzingatia kuwa kuna masoko mawili makubwa Soko la Kimataifa la Samaki Mwaloni na Soko la Matunda na mbogambogala Kirumba ambalo limehamishiwa katika uwanja wa magomeni kwa muda kupisha ujenzi wa soko jipya. Pia kuna wafanyabiashara wengi wa maduka ya jumla na rejareja pamoja na wajasiliamali wadogowadogo.
Kata ya Kirumba ina Zahanati moja ya Serikali na nyingine mbili (2) za binafsi ambazo ni zelubabeli Dispensary, pamoja Victoria Kliniki Zahanati ya Kirumba imekuwa ikitoa huduma za afya kwa kata jirani kama Kitangiri, Ibungilo na Nyamanoro,
4.0 ELIMUi) ELIMU YA MSINGI
Kata ya Kirumba ina jumla ya shule za msingi 6 na Sekondari 4 ambapo shule za Serikali 5. Shule za Serikali ni6(i) Shule ya msingi Kirumba (ii) Shule ya msingi Ziwani (iii) Shule ya msingi Songambele, (iv) Shule ya msingi Bugungumki, (v) Shule ya msingi TumainiShule za msingi zisizo za serikali ni moja (1) ambayo ni:-(i) Shule ya Msingi Bismarck(i) ELIMU SEKONDARIKata hii ina jumla ya shule za Sekondari nne ambazo ni:-(i) Shule ya sekondari Kirumba (ii) Shule ya sekondari Kabuhoro(iii)Shule ya sekondari Taqwa ambayo ni Shule ya binafsi(iv)shule ya sekondari ibanda Islami
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.