UTANGULIZI:
Idara ya Mifugo na Uvuvi inaundwa na Sehemu kuu mbili (2) ambazo ni:-
(i) Mifugo
(ii) Uvuvi.
MAJUKUMU YA IDARA:
Jukumu la Idara hii ni kutekeleza shughuli mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na Serikali kuu na Wadau kutoka Sekta binafsi. Shughuli zinazofanywa na Idara ni pamoja na:-
1.Uvuvi
Kusimamia shughuli za uvuvi wa ziwani ikiwa ni pamoja na kutoa leseni za uvuvi, kusajiri vyombo vya uvuvi, Kuhamasisha ufugaji wa samaki katika mabwawa kwa lengo la kuinua kipato na lishe, Kusimamia soko la samaki waloni Kirumba, kutoa kusimamia viwanda vya samaki na kusimamia wavuvivi kupitia vikundi vya BMUs kuhakikisha wanafanya uvuvi endelevu.
2. Maendeleo ya Mifugo
Kusimamia utekelezaji wa shughuli za Maendeleo ya mifugo na ufugaji kupitia huduma za ugani ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uundwaji wa vikundi vya wafugaji. Kusimamia na kuratibu huduma za kinga na tiba kwa mifugo zitolewazo na Halmashauri, Serikali Kuu na sekta binafsi. Kusimamia ukaguzi wa nyama na mazao yatokanayo na Mifugo usimamizi wa usafi wa mazingira ya machinjio zetu ndogo za mifugo. Kusimamia utoaji wa vibali mbali mbali vya kusafirishia mifugo na Mazao ya Mifugo ndani ya nchi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Anuani ya Posta: 735 MWANZA
Simu: + 255 736 200910
Simu:
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Haki Miliki 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.Haki zote zimeifadhiwa