Idara ya Ujenzi ina vitengo vinne vya Barabara, Majengo, Karakana na Utawala vyenye jumla ya watumishi 16, kati ya hao watumishi wa barabara ni 8, majengo 5, karakana 1 na utawala 2.
Kitengo cha barabara kinahusika na ujenzi , ukarabati na matengenezo ya barabara za Wilaya zenye urefu wa km 541.34; ujenzi , ukarabati na matengenezo ya madaraja, kalavati na drifti.
Kitengo cha majengo husimamia ujenzi na ukarabati wa majengo ya umma katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na kutoa ushauri wa kitaalam kwa majengo ya watu binafsi pale panapohitajika.
Kitengo cha Karakana kinashughulika na utengenezaji na kufanya "Service" Magari, Mitambo na Mashine mali ya Serikali.
Nidhamu ya wafanyakazi na ushirikiano miongoni mwao inaendelea/unaendelea kuimarika, vikao mbali mbali katika ngazi ya Vitengo na Idara vinafanyika kwa mujibu wa ratiba iloyowekwa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Anuani ya Posta: 735 MWANZA
Simu: + 255 736 200910
Simu:
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Haki Miliki 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.Haki zote zimeifadhiwa