HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina kitengo cha ugavi ambacho kumeundwa kwa mujibu wa sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kufugu na 37 ambapo sheria hiyo inaitaka taasisi ya serikali iwe na kiktengo cha ugavi (Procurement Management Unit –PMU).
Kitengo cha ugavi kinakiwa kiwe na mkuu wa kitengo mwenye elimu aliyosomea ujuzi huo na sifa, uzoefu katika kazi za manununzi na pia awe amesajiriwa na Bodi ya manunuzi (Procurement Professional Body).
Kwa mujibu wa sheria mkuu wa kitengo cha ugavi ataripoti moja kwa moja Afisa mashuhuri wa taasisi husika.
Afisa masuhuri wa taasisi atahakikisha kwamba kitengo cha ugavi (PMU) kinatengewa fedha kwenye bajeti ili kiweze kutimiza majukumu yake.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA UGAVI
Majukumu ya kitengo cha ugavi yameainishwa kwenye sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kipengele cha 38 kama yalivyo ainishwa hapa chini:-
Kushughulikia manunuzi yote ya taasisi
Kusaidia majukumu ya Bodi ya zabuni
Kutekeleza maamuzi ya bodi ya zebuni
Ni sekretarieti ya Bodi ya Zeburi
Kuandaa na kupitia orodha ya mahitaji
Kuandaa nyaraka za zebuni
Kuandaa matangazo ya zebuni
Kuandaa mikataba
Kutoa mikataba iliyokwisha kusainiwa
Kutunza kumbukumbu za manunuzi
Kutunza orodha au rejesta ya kikataba yote iliyoingiwa
Kuandaa taarifa ya mwezi ya bodi ya zebuni.
Kuandaa mpango wa mahitaji
Kitengo cha ugavi kinasimamia manunuzi yote toka idara na vitengo vilivyoko kwenye Halmashauri kitengo hiki kina wataalamu wanne ambao wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya manunuzi.
Aidha kitengo cha ugavi mbali na kufanyakazi na idara na vitengo vya Halmashauri, pia kinafanya kazi kwa karibu sana kwa kushirikiana na Bodi ya Zabuni ya Halmashauri ambayo majukumu yake yameainishwa na sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kifungu cha 33 (1) (a) –( e).
Nawasilisha
…………………….
Andrew E. Ndaki
Afisa ugavi – Manispaa
ILEMELA.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Anuani ya Posta: 735 MWANZA
Simu: + 255 736 200910
Simu:
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Haki Miliki 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.Haki zote zimeifadhiwa