UTANGULIZI
Idara ya Afya ni miongoni mwa idara katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela. Idara ya Afya inatekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Huduma hizi zimekuwa zikitolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya na kwa njia ya mkoba katika maeneo mbalimbali ya Manispaa. Katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuna jumla ya vituo 45 vya kutolea huduma za afya. Vituo hivi vinamilikiwa na serikali, watu binafsi, mashirika ya dini pamoja na taasisi za serikali. Vituo vya kutolea huduma za Afya vinavyomilikiwa na serikali ni 15, Vituo 21 vinamilikiwa na watu binafsi, 4 vinamilikiwa na mashirika ya dini na vituo 5 vinamilikiwa na taasisi za serikali. Kati ya vituo hivyo 45, kuna hospitali 1, vituo vya Afya 12 na zahanati 32.
Idara ya Afya inatekeleza majukumu makuu mawili abayo ni Afya kinga na Afya tiba. Kupitia Afya tiba idara imelenga kutoa matibabu sahihi kwa gharama nafuu kwa wananchi wa Manispaa ya Ilemela pamoja na Wilaya za jirani. Afya kinga imelenga kuwakinga wananchi wasipate magonjwa yale ya kuambukiza, yasiyoyakuambukiza pamoja na kuzuia magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Idara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na kutekeleza mpango mkakati wa afya wa V wa mwaka 2015 -2020. Katika kuhakikisha wananchi wanapata tiba sahihi, idara imekuwa ikitekeleza majukumu yafuatayo:
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Anuani ya Posta: 735 MWANZA
Simu: + 255 736 200910
Simu:
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Haki Miliki 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.Haki zote zimeifadhiwa